Saturday, September 17, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, AKABIDHIWA MSAADA WA DOLA LAKI MBILI UTOKA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) taslimu kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.