Thursday, September 29, 2016

RONALDO ARUDI KIKOSI CHA MABINGWA WA ULAYA PORTUGAL

Cristiano Ronaldo ametajwa kuwemo miongoni mwa Kikosi cha Portugal kwa ajili ya Mechi za Kundi B la Nchi za Ulaya zinazowania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi B, Porugal, wakicheza bila Majeruhi Ronaldo, walichapwa 2-0 Ugenini na Switzerland mapema Mwezi huu.
Kocha wa Portugal, Fernando Santos, ameeleza kuwa Kikosi chake kinakuwa na nguvu zaidi ikiwa Ronaldo yumo.
Ronaldo, mwenye Miaka 31, aliukosa mwanzo wa Msimu Mpya huu wa La Liga akijiuguza Goti kwenye Fainali ya EURO 2016 Julai 10 ambayo Portugal walibeba Kombe na kuwa Mabingwa wa Ulaya.
Mbali ya Ronaldo, Wachezaji wengine waliorejeshwa Kikosini baada ya kuikosa Mechi na Switzerland ni Renato Sanches wa Bayern Munich, Andre Gomes wa Barcelona na Kipa Anthony Lopes wa Lyon.
Kwenye Mechi za Kundi B la Nchi za Ulaya zinazowania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, Portugal watakuwa Wenyeji wa Andorra hapo Oktoba 7 na Siku 3 baadae kwenda Ugenini kucheza na Faroe Islands.

Portugal – Kikosi kamili:
Makipa: Rui Patricio (Sporting), Anthony Lopes (Lyon/FRA), Marafona (Braga);

Mabeki:
Antunes (Dynamo Kiev/UKR), Bruno Alves (Cagliari/ITA), Cedric Soares (Southampton/ENG), Jose Fonte (Southampton/ENG), Joao Cancelo (Valencia/ESP), Pepe (Real Madrid/ESP), Raphael Guerreiro (Dortmund/GER);

Viungo: Adrien Silva (Sporting), William Carvalho (Sporting), Andre Gomes (Barcelona/ESP), Danilo Pereira (FC Porto), Joao Mario (Inter Milan/ITA), Joao Moutinho (Monaco/FRA), Renato Sanches (Bayern/GER)
Mafowadi: Cristiano Ronaldo (Real Madrid/ESP), Andre Silva (FC Porto), Bernardo Silva (Monaco/FRA), Eder (Lille/FRA), Gelson Martins (Sporting), Nani (Valencia/ESP), Ricardo Quaresma (Besiktas/TUR)