Thursday, September 22, 2016

SERENGETI BOYS WAPAA LEO

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys imepaa kwenda Kigali, Rwanda ambako itaweka kambi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Kongo.
Serengeti Boys inajiandaa mechi wa marudiano kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Congo Brazaville ambao kwenye mchezo wa awali walifungwa mabao 3-2 jijini Dar es Salaam.
"Timu imeondoka saa 3.00 asubuhi kwenda Kigali, Rwanda. Itafika saa 4.30 asubuhi kwa mujibu wa ratiba," alisema Alfred Lucas Mapunda, Msemaji wa TFF.