Sunday, September 18, 2016

SERENGETI BOYS YAIFUNGA 3-2 CONGO BRAZZAVILLE


Wachezaji wa timu ya taifa ya Soka ya Vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' wakishangilia bao lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Yohana Mkomola katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenzao wa Congo Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Serengeti Boys imeshinda 3-2. (Picha zote na Francis Dande)

Mashabiki wa soka wakishangilia timu ya taifa ya Soka ya Vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys'.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akishanglia na mashabiki wa soka waliofika kushuhudia pambano la timu ya taifa ya Soka ya Vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' ilipopambana na Congo Brazzaville.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwapungia mkono mashabiki wa soka.
Mfungaji wa mabao 2 ya Serengeti Boys, Yohana Mkomola akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili.
Wachezaji wa Serengeti Boys wakishangilia bao la tatu la timu hiyo.
Furaha ya ushindi.
Wakishagilia.
Golikipa wa Congo Brazzaville, Obouua Examish Yawn akiokoa hatari langoni mwake.
Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Mohamed Rashid Abdallah akichuana na beki wa Congo Brazzaville.
Waamuzi wakitoka baada ya kumalizika kwa mchezo huo.