Wednesday, September 14, 2016

TAMASHA LA UHONDO WA ZANTEL LAKONGA NYOYO ZA WAKAZI WA TMK


Msanii wa muziki wa bongo flava, Seif Mwinjuma ‘sholo mwamba’ akiimba katika tamasha la Uhondo wa Zantel lililofanyika katika viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam hivi karibuni ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo sokoni.

Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wakazi wa Temeke, Dar es Salaam kuhusu huduma na bidhaa mpya zitolewazo na kampuni hiyo wakati wa tamasha lililopewa jina la ‘uhondo wa Zantel’ lililodhaminiwa na kampuni hiyo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ally Momba ‘Momba’ akionyesha umahiri wake wa kuimba katika tamasha la Uhondo wa Zantel lililofanyika katika viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo sokoni.

Msanii maarufu anayetesa na wimbo wake wa ‘segere’ Siza Mazongela
akikonga nyoyo za mashabiki wake katika tamasha la Uhondo wa Zantel
lililofanyika katika viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam
ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu yamkononi ya Zantel kuwa
karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo
sokoni.