Monday, September 12, 2016

TASWA FC NA TASWA SC ZATAMBA KATIKA BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI JIJINI ARUSHA

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha kwenye uwanja wa General Tyre jumapili, kulia ni Mwenyekiti wa Taswa FC,Majuto Omary na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma. Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)