Tuesday, September 13, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: PSG 1 v 1 ARSENAL, GIROUD NA VERRATTI WOTE WAONESHWA NYEKUNDU KUKOSA MECHI ZIJAZO!


Paris St Germain 1 vs 1 Arsenal
Huko Parc des Princes, Paris, Nchini France, Edinson Cavani aliipa Bao PSG baada ya Sekunde 42 tu toka Gemu ianze lakini Alexi Sanchez alisawazisha na kuipa Arsenal Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kundi A.

Mechi hii iliisha kwa kila Timu kubaki Mtu baada ya Olivier Giroud na Verratti kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya wote kupewa Kadi za Njano za Pili baada ya kuvaana Dakika za mwishoni.