Sunday, September 25, 2016

VPL FULL TIME: STAND UNITED 1 v 0 YANGA, PASTORY ATHANAS AWASIMAMISHA KASI YANGA SHINYANGA LEO!

MABINGWA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga Leo huko Kambarage, Shinyanga wameomja kipigo chao cha kwanza Msimu huu kwa kufungwa 1-0 na Stand United.
Bao ambao limewazamisha Yanga lilifungwa Dakika ya 58 na Athanas Pastory.
Ushindi huo umewainua Stand United hadi Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 12 zikiwa ni Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba wenye Pointi 16 huku wote wakiwa wamecheza Mechi 6 kila mmoja.

Yanga, ambao wamecheza Mechi 5, wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 10, wakifuata Azam FC wenye Pointi 10 lakini wamecheza Mechi 6.
Katika Mechi nyingine ya VPL iliyochezwa huko Mabatini, Mlandizi, Ruvu Shooting na Toto Africans zilitoka 0-0.

VPL itaendelea Jumatatu kwa Mechi 1 kati ya African Lyon na Kagera Sugar.
Mechi inayofuata kwa Mabingwa Yanga ni Dabi ya Kariakoo dhidi ya Mahasimu wao Simba hapo Jumamosi Oktoba Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Timu hiyo inatarajia kung’oka Shinyanga kwenda Visiwani Pemba kujipanga upya kwa kitimitim chao na Vinara Simba.
Pastor  Athanasi dakika ya 58 antipathy Stand bao la kuongoza dhidi ya  Yanga sasa ni 1-0