Beki wa timu ya Wabunge Mashabiki wa Simba, William Ngeleja akijaribu kumzuia mshambuliaji wa timu ya Wabunge Mashabiki wa Yanga, Rizawan Kikwete katika mchezo wa Hisani wa kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Wabunge Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Mwigulu Nchemba.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Kombe nahodha wa timu ya Wabunge Mashabiki wa Yanga, Ahmed Nguali bara baada ya kuwafunga 5-2 Wabunge Mashabiki wa Simba katika Mechi ya Hisani ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba,
Wabunge Mashabiki wa Yanga wakishangilia ubingwa wa Mechi ya Hisania kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba, baada ya kuwachapa Wabunge Mashabiki wa Simba kwa mabao 5-2 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.