Sunday, September 18, 2016

WAPENZI WA SOKA KUNUFAIKA NA ‘SOKA BANDO’ KUTOKA VODACOM

Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara , “Vodacom Premier League” imesikia kilio cha mashabiki na wapenzi wa soka nchini na kuamua kuwaletea kifurushi maalumu kinachojulikana kama ‘Soka bando’ ambacho ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote.
Vodacom Tanzania imebuni kifurushi hiki kwa ajili ya kuwapatia taarifa za soka za hapa nchini na ligi za kimataifa kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-Kifurushi cha ‘Soka bando’ kitakuwa kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa saa 24.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella amesema “Kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-mashabiki wa soka wanaotumia mtandao wa Vodacom watapata taarifa mbalimbali za soka za hapa nyumbani na kimataifa kwa kipindi cha siku 7,dakika 14 za muda wa maongezi Vodacom kwenda Vodacom, dakika 2 za muda wa maongezi kwa mitandao yote na jumbe fupi za maneno (SMS) 20 kwa kipindi cha masaa 24”
Alisema Vodacom Tanzania imeleta kifurushi hiki cha ‘Soka bando’ kipindi hiki ambacho msimu wa ligi ya VPL unaendelea ni furaha kwa Mtandao wa Vodacom kuwawezesha mashabiki kupata taarifa za ligi kwa urahisi kupitia mtandao wake ikiwemo kuwapatia burudani wateja wake na watanzania wote kwa ujumla.

“Kampuni inathamini na kutambua mchango wa mashabiki katika kukuza ligi hii tangu ilipoanza kuidhamini hivyo ndio maana tumewaletea kifurushi hiki ili wapate burudani na taarifa za soka kwa wakati na kwa gharama nafuu”.Alisema Mwiyombella.
Ili kununua kifurushi hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga namba *149 * 01#, na kuchagua ‘Soka Bando’. Baada ya hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga” “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya Mspoti.vodacom.co.tz.
Wateja watakaojiunga na huduma hii pia watapata nafasi ya kufurahia ofa na zawadi mbalimbali kutoka Vodacom kama vile muda wa bure wa maongezi, sms au MB za kuperuzi inteneti hususani timu wanazoshabikia zitakapokuwa zimeibuka na ushindi wa mchezo.
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya VodacomTanzania bara unaendelea katika viwanja mbalimbali nchini.