Saturday, September 24, 2016

WASANII WA KAGERA WAJITOKEZA KWA WINGI KUJITOLEA DAMU KWA WATU WALIOATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI LEO KWENYE UWANJA WA UHURU PLATFORM BUKOBA.Wasanii mbalimbali Mkoani Kagera wamejitokeza katika uwanja wa Mashujaa maarufu kwa jina la Mayunga mjini Bukoba kujitolea damu kwa ajili ya majeruhi wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10.
Akizungumzia zoezi hilo Mwenyekiti wao Onyango Ochola alisema ni kawaida yao kushiriki matukio mbalimbali ya kijamii ikiwemo kujitolea kuoko maisha ya watu wengine kama majeruhi wa tukio hilo.Alisema msaada wanaoweza kuutoa kwa sasa kama wasanii ni kujitokeza kuchangia damu siku ya Jumamosi na kuwa hata miongoni mwa waathirika ni ndugu wa wasanii na wafuatiliaji wa kazi zao hivyo wanaona fahari kushiriki kuokoa uhai wa watu wengine.

‘’Hatuna kitu tunachoweza kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi hasa wale awaliojeruhiwa zaidi ya kujitolea damu ili kuokoa maisha yao,miongoni mwa waliojeruhiwa wamo ndugu wa wasanii na mashabiki wetu’’alisema Ochola


Naye katibu msaidizi wa wasanii hao Bama Crosper alisema kuwa tukio la kujitokeza kujitolea damu litawasogeza karibu zaidi na jamii ambayo hufuatilia kazi zao na kutaka watu wa makundi mbalimbali wajitokeze kuwaunga mkono.