Monday, October 31, 2016

BONDIA THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA KWA KUSHAMBULIWA NA WATU WASIOJULIKANA

Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika),amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony Lutta,ameiambia blogu hii kwamba, taarifa walizozipata ingawa bado hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa.
Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui nini kimempata ambapo mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya taifa muhimbili.
Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi.
Mashali ambaye jina lake la kuzaliwa ni Christopher Fabian Mashali,aliyezaliwa Septemba 09 mwaka 1989,ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO,amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.
Marehemu ameacha mke na watoto