Thursday, October 27, 2016

EFL CUP – DROO YA ROBO FAINALI: YAFANYIKA, MAN UNITED v WEST HAM UNITED, ARSENAL v SOUTHAMPTON...

DROO ya Mechi za Robo Fainali ya EFL CUP, Kombe la Ligi la England, imefanyika hii Leo mara baada ya Mechi ya mwisho ya Raundi ya 4 ambayo Man United iliwabwaga Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Man City 1-0 huko Old Trafford.
Katika Droo hiyo, Vigogo wote wa Ligi Kuu England waliobakia kwenye Mashindano haya wamepangwa kucheza Mechi zao Viwanja vya Nyumbani kwao na hiyo ni faida kubwa kwao.

DROO KAMILI:
Man United vs West Ham
Liverpool vs Leeds United 

Arsenal vs Southampton
Hull City vs Newcastle


JE WAJUA? -Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.


Mechi za Robo Fainali zitachezwa Wiki ya kuanzia Novemba 28.