Monday, October 24, 2016

EFL CUP: RAUNDI YA 4 JUMANNE, ARSENAL v READING, LIVERPOOL v SPURS. JUMATANO OLD TRAFFORD MAN UNITED v MAN CITY

RAUNDI ya 4 ya EFL CUP ambalo ndio Kombe la Ligi huko England itachezwa Jumanne kwa Mechi 5 na Jumatano Mechi 3.
Kati ya Mechi hizo za Jumanne zipo za Arsenal na Reading Uwanjani Emirates na ile kali kabisa huko Anfield kati ya Liverpool na Tottenham.
Jumatano zipo Mechi 3 na zote kushirikisha Timu za Ligi Kuu England pekee ambapo Southampton wataikaribisha Sunderland huko Saint Mary na West Ham kuwa Wenyeji wa Chelsea kati Dabi ya Timu za London wakati Jijini Manchester ipo Dabi ya Jiji hilo Uwanjani Old Trafford kati ya Manchester United na Manchester City.

Washindi 8 wa Raundi ya 4 watasonga na kutinga Robo Fainali ambapo Droo yake itafanyika mara tu baada ya Mechi ya mwisho hapo Jumatano. Bingwa Mtetezi wa Kombe la Ligi ni Man City ambao walitoka Sare 1-1 na Liverpool na kutwaa Kombe kwa Matuta.

EFL CUP
Raundi ya 4 

Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
Jumanne Oktoba 25
Arsenal v Reading
Bristol City v Hull
Leeds v Norwich
Liverpool v Tottenham
Newcastle v Preston

Jumatano Oktoba 26
Southampton v Sunderland
West Ham v Chelsea

 2200 Man United v Man City