Saturday, October 22, 2016

EPL: LIVERPOOL 2 v 1 WESTBROMWICH ALBION

Liverpool waliifunga West Brom 2-1 huko Anfield kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England lakini wameshindwa kuing'oa Arsenal kileleni kutokana na Bao hilo moja walilofungwa hiyo Jana.
Liverpool walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 20 Mfungaji akiwa Sadio Mane na la Pili Dakika ya 35 kupitia Philippe Coutinho.
WBA walipata Bao lao pekee Dakika ya 81 ambalo alifunga McAuley.
Kama Liverpool wangeshinda 2-0 basi wangeipiku Arsenal toka kileleni mwa EPL.
Jana Arsenal walitoka 0-0 na Middlesbrough na kukaa kileleni wakiwa Pointi 1 mbele ya Man City ambao Leo wapo kwao Etihad kucheza na Southampton.
Mechi nyingine hii Leo ni huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na Man United.