Thursday, October 20, 2016

EUROPA LEAGUE LIVE: MANCHESTER UNITED 4 v 1 FENERBAHCE


Man United walibadilisha Wachezaji 7 toka Kikosi kilichoanza Mechi na Liverpool Jumatatu iliyopita, Manchester United Leo wameitandika Fenerbahce ya Uturuki Bao 4-1 Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya 3 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 31 kwa Penati ya Paul Pogba iliyotolewa baada ya Pasi ndefu ya Michael Carrick kumkuta Juan Mata ambae aliangushwa na Simon Kjaer.
Dakika 2 baadae Man United wakafunga Bao lao la Pili kwa Penati nyingine iliyopigwa na Anthony Martial baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Sener Ozbayrakli wakati akichanja mbuga kumuona Kipa alipoinasa Pasi ya Juan Mata.

Bao la 3 lilipigwa Dakika ya 45 kufuatia Rooney kuunasa Mpira na kumpasia Jesse Lingard aliemtengea Paul Pogba na kuachia kigongo cha Mita 20 hadi wavuni.
Hadi Mapumziko Man United 3 Fenerbahce 0.
Dakika 3 baada ya Kipindi cha Pili kuanza, Man United waliandika Bao la 4 kwa Mpira ulioanza kwa Paul Pogba aliempasia Wayne Rooney ambae alimsogezea Jesse Lingard alieachia Shuti kali toka Mita 20 na kuingia wavuni.
Dakika ya 83, Robin van Persie, Mchezaji wa zamani wa Man United, aliipa Fenerbahce Bao lao pekee alipounganisha Krosi ya Emenike.

Van Persie mchezaji wa zamani wa Man United sasa akikipiga kwenye klabu yake mpya ya Fenerbahce na usiku huu anaungana na Wachezaji wake wa Klabu ya Man United kukinukisha kwenye Ligi ya Europa Ligi.