Thursday, October 20, 2016

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO JUU, GERMANY, BRAZIL ZAIKARIBIA, TANZANIANI YA 144

FIFA Leo imetoa Listi ya Ubora Duniani na Vinara wamebaki Argentina lakini sasa wanakaribiwa na Mabingwa wa Dunia Germany na Brazil waliopanda kuchukua Nafasi za Pili na za Tatu wakati Beligium ikishuka Nafasi 2.
Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka Nafasi 12.
Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio Nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32.

Listi nyingine ya Ubora itatolewa Novemba 24.
20 BORA:
1. Argentina
2. Germany
3. Brazil
4. Belgium
5. Colombia
6. Chile
7. France
8. Portugal
9. Uruguay
10. Spain
11. Wales
12. England
13. Italy
14. Switzerland
15. Poland
16. Croatia
17. Mexico
18. Costa Rica
19. Ecuador
20. Netherlands