Saturday, October 29, 2016

FULL TIME EPL: SUNDERLAND 1 v 4 ARSENAL

Arsenal wakicheza Ugenini huko Stadium of Light kwenye Mechi yakwanza ya EPL, Ligi Kuu England, hii Leo waliitandika Timu ya Mkiani Sunderland Bao 4-1 na kutwaa uongozi wa Ligi hiyo wakiiacha Sunderland ikiwa mkiani.
Uongozi huu wa Arsenal huenda ukadumu hadi Mechi ya Manchester City ambao wakishinda zaidi ya Bao 3 dhidi ya West Bromwich Albion watatwaa tena uongozi wa EPL.Arsenal walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 19 kwa Krosi ya Oxlade-Chamberlain kuunganishwa kwa Kichwa na Alexis Sanchez.
Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili Krosi ndefu ya Ndong wa Sunderland ilimkuta Watmore aliemhadaa Sentahafu Mustafi na kumzunguka Kipa Cech ambae alimwangusha Watmore na Refa Atkinson kutoa Penati iliyofungwa na Jermaine Defoe katika Dakika ya 65.
Dakika ya 70, Arsene Wenger aliamua kumtoa Alex Iwobi na kumwingiza Olivier Giroud ambae alifunga Bao 2 Dakika za 71 na 75.
Arsenal walifunga Bao lao la 4 Dakika ya 78 kupitia Alexis Sanchez.