Sunday, October 30, 2016

FULL TIME: SOUTHAMPTON 0 vs 2 CHELSEA

CHELSEA, wakicheza Ugenini huko Saint Mary, wameichapa Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, Bao 2-0 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England,
Chelsea waliandika Bao lao la kwanza Dakika ya 6 kupitia Eden Hazard aliepata Pasi Moses.
Bao hilo lilidumu hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili Dakika ya 55 Diego Costa aliipa Chelsea Bao la Pili kwa Shuti kali la kupinda toka nje ya Boksi.
Ushindi huu umewapaisha Chelsea hadi Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Vinara Timu 3 zinazofungana kwa Pointi, Man City, Arsenal na Liverpoool.
Katika Mechi ya awali ya EPL iliyochezwa mapema hii Leo huko Goodison Park, Wenyeji Everton waliifunga West Ham 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Pili.
Romelu Lukaku aliipa Everton Bao la Kwanza Dakika ya 50 kwa Kichwa na Ross Barkley kupiga la Pili Dakika ya 76.