Saturday, October 29, 2016

FULL TIME: WEST BROMWICH 0 v 4 MANCHESTER CITY

WEST BROM 0 MAN CITY 4
Man City wameipiga WBA Bao 4-0 na kurejea kileleni mwa EPL ambako walikaa Arsenal kwa muda hii Leo baada ya kuwafunga Sunderland 4-1 mapema Leo.
Sergio Aguero aliwapa City Bao Dakika ya 19 baada kupokea Pasi ya Ilkay Gundogan.
Aguero tena aliipa City Bao la Pili Dakika ya 27 kwa Shuti kali ambalo lilimshinda Kipa Ben Forster.
Hadi Mapumziko WBA 0 City 2.
Dakika ya 79 City walifunga Bao lao la 3 Mfungaji akiwa Ilkay Gundogan alipopokea pasi safi ya Sergio Aguero.
City walipiga Bao lao la 4 Dakika ya 89 kupitia Kevin De Bruyne alietokea Benchi.