Sunday, October 2, 2016

FULL TIME....MANCHESTER UNITED 1 v 1 STOKE CITY

Jose Mourinho arrives Old Trafford 20161002Ligi Kuu England, inaendelea Leo kwa Mechi 4 na ya kwanza kabisa ni huko Old Trafford kati ya Manchester United na Stoke City.

Baada ya kupata ushindi mnono walipoitwanga Leicester City 4-1 na kufuatia Juzi kuifunga Zorya Luhansk kwenye UEFA EUROPA LIGI huku Wachezaji wao Ander Herrera, Marcus Rashford na Zlatan Ibrahimovic wakicheza vizuri Man United sasa nguvu zao zipo kwa Stoke ambao Msimu huu wanayumba vibaya wakiwa chini ya Meneja Mark Hughes Mchezaji wa zamani wa Man United.

Kwa sasa Stoke, ambao Pointi zao za EPL ni kutoka kwenye Droo zao mbili dhidi ya West Brom and Middlesbrough na kufungwa Mechi 4, wapo mkiani mwa Ligi hii wakati Man United wapo Nafasi ya 7 na ushindi utawapaisha hadi Nafasi ya 3.

Jose Mourinho, Meneja wa Man United, amesema Majeruhi pekee kwake nin Phil Jones wakati Luke Shaw na Henrikh Mkhitaryan wamepona na wanaweza kurejea Kikosini.

Kwa Miaka 40, na hasa baada ya Stoke kupanda Daraja Mwaka 2008 kuingia EPL, Man United wameitwanga Stoke Mechi zote zilizochezwa Old Trafford wakifunga Jumla ya Mabao 25 huku Wayne Rooney akipiga Bao 4 kati ya hizo.