Monday, October 31, 2016

GARETH BALE ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA 6 REAL, UKITAKA KUMNUNUA LIPA EURO MILIONI 500

Gareth Bale amesaini Mkataba Mpya na Klabu yake ya Spain Real Madrid ambao utamweka hapo kwa Miaka 6 zaidi.
Bale, Raia wa Wales mwenye Miaka 27, alijiunga na Real kutoka Tottenham Hotspur Mwaka 2013 kwa Dau la Rekodi ya Dunia wakati huo la Pauni Milioni 86.
Akiwa na Real, Bale amefanikiwa kutwaa UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI mara 2 na kujijenga mno Kimpira.
Bale ameifungia Real Mabao 62 katika Mechi 134 na Msimu uliopita alikuwemo kwenye Kikosi cha Msimu cha UCL.

Hivi sasa Real imefanikiwa kuwafunga upya kwa Mikataba mipya Wachezaji wao wengine Luka Modric, Lucas Vazquez na Toni Kroos na anaefuatia ni Cristiano Ronaldo.
Klabu ya Real ilithibitisha taarifa hizi za Bale kwa kutangaza kuwa Gareth Bale atakuwa na Mkutano na Wanahabari Jumatatu Oktoba 31 ili kutangaza kwake kubakia Real hadi Juni 30, 2022.

Pamoja na kuongeza Mkataba, pia imedokezwa kuwa Mkataba huo Mpya wa Bale unacho Kipengele ambacho kinataka Klabu inayotaka kumnunua ndani ya Mkataba huo illipe Euro Milioni 500 ili aweze kuihama Real kabla ya Juni 39, 2022.