Tuesday, October 4, 2016

JAMHURI KIWELU JULIO ASEMA AMECHOSHWA NA MATENDO YA WAAMUZI WA SOKA NCHINI! ATANGAZA KUKAA MBALI NA SOKA!


Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio, October 2 2016 ametangaza kujiuzulu kufundisha soka la nchini Tanzania kufuatia kutoridhishwa na maamuzi yanayofanywa na marefa uamuzi huo umeonekana kuwashtua walio wengi, hiyo ni baada ya kupata kichapo kutoka kwa Mbeya City akiwa katika uwanja Sokoine Mbeya kwa kupoteza kwa goli 1-0. Jamhuri Kiwelu Julio baada ya mechi hiyo aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa saivi atakuwa anaenda kuangalia mpira uwanjani ila hawezi tena kuwa kocha wa mpira Tanzania. “Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu