Saturday, October 22, 2016

KAGERA SUGAR v YANGA LEO UWANJA WA KAITABA BUKOBA

LEO zipo Mechi 6 za VPL, Ligi Kuu Vodacom, na moja ni ile ya Mabingwa Watetezi Yanga ambao wapo Ugenini huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kucheza na Kagera Sugar.
Mechi nyingine 5 za Leo ni mbili zitakazochezwa Jijini Dar es Salaam wakati Azam FC wakicheza na JKT Ruvu juko Azam Complex, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Saa 1 Usiku na ya pili ni ile ya Uwanja wa Uhuru kati ya African Lyon na Mbeya City.

Mechi nyingine ni huko Manungu, Morogoro kati ya Wenyeji Mtibwa Sugar na Stand United na huko Songea kati ya Maji Maji FC na Ruvu Shooting.

Hadi sasa Simba ndio wapo kileleni mwa VPL sasa wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi 10 baada ya kushinda Mechi 8, Sare 2 na Kutofungwa.

Timu ya Pili ni Stand United wenye Pointi 20 kwa Mechi 11 na wa 3 ni Yanga wenye Pointi 18 kwa Mechi 9.

Jumapili Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Mbao FC.