Friday, October 7, 2016

KAGERA SUGAR WAKUBALI KICHAPO CHA BAO 2-0 KUTOKA KWA TOTO AFRICAN LEO KAITABA.

TOTO AFRICANS ya Mwanza Leo hii imeibuka kidedea huko Kaitaba, Bukoba kwa kuifunga Kagera Sugar 2-0 kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom.
Wakicheza Mechi yao ya kwanza chini ya Kocha wao wa zamani Khalfan Ngassa, Toto walipata ushindi wao kwa Bao za Dakika za 47 na 80 zilizofungwa na Jamal Sudi na Mohammed Soud.

Ngassa amekamata wadhifa huu baada ya kuondoka kwa Kocha Rogasian Kaijage.
Ushindi huu umewaweka Toto Nafasi ya 11 wakiwa na Pointi 8.

Huko Sokoine Mjini Mbeya, Mechi nyingine ya VPL kati ya Mbeya City na Stand United ilimalizika kwa Sare ya 0-0.