Monday, October 17, 2016

LEO NDANI YA ANFIELD, LIVERPOOL v MANCHESTER UNITED

LEO Saa 4 Usiku, Saa za Bongo, Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool utakuwa kitovu cha Dunia nzima kushuhudia mtanange mkali wa EPL, Ligi Kuu England kati ya Mahasimu wa Jadi Liverpool na Manchester United.
Kuzizima kwa mtanange huu kumefanya Klabu zote mbili ziwaonya Mashabiki kutofanya vitendo vya kihuni.
Wakati Man United imethibitisha Wachezaji wao wote wako fiti, Liverpool inao Wachezaji kadhaa wenye maumivu.
Miongoni mwa hao ni Georginio Wijnaldum, Adam Lallana, Dejan Lovren, Roberto Firmino, Philippe Coutinho na Nathaniel Clyne.
Lakini Meneja wa Liverpool Jurgen Kloop amethibitisha Wijnaldum na Lallana hawapo nje ya Gemu hii.

Hadi sasa, baada ya Mechi 8, Man City na Arsenal ndizo zipo kileleni zikiwa na Pointi 19 kila mmoja na wanafuata Suprs wenye Pointi 18, kisha Liverpool wenye Pointi 16 kwa Mechi 7 wakiwaxsawa na Chelsea waliocheza Mechi 8.
Nafasi ya 6 inashikwa na Everton wenye Pointi 15 kwa Mechi 8 na wa 7 ni Man United wenye Pointi 13 kwa Mechi 7.


Msimu uliopita kwenye EPL, Man United iliipiga Liverpool nje ndani kwa kuichapa 1-0 huko Anfield hapo Januari 1, 2016 na kushinda 3-1 huko old Trafford hapo Septemba 12, 2015.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
LIVERPOOL: Karius, Clyne, Lovren, Matip, Milner, Henderson, Coutinho, Wijnaldum, Mane, Firmino, Lallana

MAN UNITED: De Gea, Valencia, Bailly, Smalling, Shaw, Herrera, Pogba, Mata, Lingard, Ibrahimovic, Rashford
REFA: Anthony Taylor

JE WAJUA?
-Mtanange wa Liverpool dhidi ya Manchester United ni pambano kubwa Duniani linalotazamwa na Watu Milioni 700 kwenye Nchi 200.

JE WAJUA?
-Uso kwa Uso:

-Liverpool Ushindi 75 Sare 62 Man United Ushindi 87