Sunday, October 2, 2016

FULL TIME ...BURNLEY 0 v 1 ARSENAL

BAO la Dakika ya 93 linalosadikiwa kuwa ni la mkono limewapa ushindi wa 1-0 Arsenal walipocheza Ugenini huko Turf Moor na Burnley.
Bao hilo lilitokana na Kona ya Mesut Ozil na Theo Walcott kupiga Kichwa na kumkuta Alex Oxlade-Chamberlain ambae alirejesha Mpira Golini na kumgonga Mkononi Laurent Koscielny na kutinga.
Mbali ya kuwa ni Mkono, Bao hilo pia limezua utata wa Ofsaidi kwa Laurent Koscielny wakati Mpira ukimgonga na pia Dakika za Nyongeza 2 kumalizika wakati linafungwa.

Ushindi huu umewaweka Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Man City.