Saturday, October 29, 2016

FULL TIME EPL.. MANCHESTER UNITED 0 vs 0 BURNLEY, MAN U WABANWA MBAVU NYUMBANI OLD TRAFFORD!!

Jose MourinhoLeo ilishuhudia Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ya upande mmoja ambayo Man United walitawala na kukosa Mabao mengi huku Difensi na Kipa wa Burnley Tom Keaton kuwa Shujaa mkubwa.
Mechi hii ilikuwa 0-0 hadi Mapumziko licha ya Man United kutawala na kutengeneza nafasi nyingi ambazo baadhi Kipa Tom Heaton, ambae alikuwa Man United, kuziokoa vizuri.
Katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza Refa Mark Clattenburg aliiminya Man United Penati pale Fulbeki on Flanagan, alieingizwa Dakika ya 43 kumbadili Stephen Ward, kumkwatua Matteo Darmian.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Meneja wa Man United Jose Mourinho kutupwa Jukwaani kwa Watazamaji na Refa Clattenburg kwa madai ya kuja juu akilalamikia Penati.
Man United walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 68 kufuatia Kadi ya Njano ya Pili kwa Ander Herrera.
Lakini waliendelea kutawala bila kufunga.
JOSE IBRAHIMOVICMASHABIKI WA BURNLEY