Saturday, October 22, 2016

FULL TIME...ARSENAL 0 vs 0 MIDDLESBROUGH, GUNNERS WAKIWA KWAO WALAZIMISHWA SARE! WENGER APAGAWA!

Arsenal leo imefanikiwa kutwaa uongozi wa EPL, Ligi Kuu England, pengine kwa Masaa 24 tu, baada ya kutoka 0-0 na Middlesbrough, maarufu kama Boro, Uwanjani Emirates.

Matokeo hayo yamemaliza wimbi la ushindi wa Mechi 6 mfululizo lakini yamewapa uongozi wa Pointi 1 mbele ya Timu ya Pili Man City ambayo Kesho ipo kwao Etihad kucheza na Southampton na ushindi au Sare itawarejesha kileleni.
Kwenye Mechi nyingine za Leo, Bao la Dakika ya 90 la Scott Arfield liliwapa Burnley ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton waliotawala Mechi hii.

Nae Xherdan Shaqiri alifunga Bao 2 nakuwapa Stoke City ushindi wa Ugenini wa 2-0 walipocheza na Hull City.

Nao Mabingwa Watetezi Leicester City, wakiwa kwao King Power Stadium, waliitandika Crystal Palace 3-1 kwa Bao za Ahmed Musa, Shinji Okazaki na Christian Fuchs huku Palace wakifunga kupitia Yohan Cabaye.

West Ham, wakiwa Nyumbani, waliitungua Sunderland 1-0