Friday, October 21, 2016

MOURINHO AWAKANDYA WANAOMPONDA POGBA, POGBA ATOBOA ROONEY KUMRUHUSU KUPIGA PENATI!

José Mourinho amewajia juu ‘wajuaji’, aliowaita “Einsteins”, ambao walimnanga Paul Pogba na kumwita ‘Mchezaji Mbovu’ EPL, Ligi Kuu England baada ya Kungo huyo kutoka France kufunga Bao 2 Jana wakati Manchester United inaichapa Fenerbahce 4-1 kwenye Mechi ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI Uwanjani Old Trafford.
Pogba alifunga Penati ya Dakika ya 31 na Bao jingine ni Kombora la Mita 25 wakati Bao nyingine zikifungwa kwa Penati ya Anthony Martial na Shuti la Mita 25 la Jesse Lingard.
Robin van Persie, Mchezaji wa zamani wa Man United, ndie aliefunga Bao pekee la Fenerbahce.
Wakati Wachambuzi na Wanahabari huko England wakimnanga Pogba kwa kufifia kwenye Mechi ya Jumatatu iliyopita huko Anfield walipotoka 0-0 na Liverpool, Jana Mourinho alijibu mapigo.
“Kwanza kabisa, kutoka kwenye Vinywa vya baadhi yenu, ametoka toka Mchezaji mbovu kabisa wa Ligi Kuu na Leo ni Mchezaji Bora ndani ya Masaa 48. Sisemi ni wewe, nasema ni Wanahabari, hasa wale Einsteins. Sisi tunajua ni Mchezaji mzuri sana. Tunajua anahitaji muda. Nalijua Soka la Italy vizuri sana, Najua Timu zinacheza tofauti kabisa toka Ligi Kuu. Sisemi sisi ni bora lakini tupo tofauti sana. Tuna tofauti ya kukamia Gemu, Mchezaji kugusa Mpira mara ngapi, kila kitu ni tofauti na anahitaji muda kubadilika. Lakini ni Kijana anaejiamini. Hatetereki kwa sa babu Watu wanamsema ni mbovu. Hakufedheheka. Alitulia. Ni vyema Mchezaji kufunga, tena kufunga Nyumbani na hasa Bao zuri sana kama lile!”

Nae Pogba ametoboa kuwa Wayne Rooney, aliekuwa akianza Mechi yake ya kwanza tangu Mwezi uliopita Man United walipoifunga Northampton 3-1 kwenye EFL CUP, ndie alimruhusu kupiga Penati aliyofunga Bao la Kwanza.
Pogba alitoboa: “Ilikuwa ni Wazza au mimi kuipiga Penati ile. Nikamwambia nataka kupiga mimi na akaruhusu. Nilifurahi na nikafunga. Kwa Mchezaji kama yeye, Kepteni wa Timu, kuniruhusu kupiga Penati, ni heshima kubwa kwake. Nimefurahi sana kwa hilo!”


MAN UNITED – Mechi zao:
Oktoba 2016
EPL, Ligi Kuu England
Jumapili Oktoba 23

1800 Chelsea v Man United
EFL Cup – Raundi ya 4
Jumatano Oktoba 26
2200 Man United v Man City
EPL, Ligi Kuu England


Jumamosi Oktoba 29
1700 Man United v Burnley
Novemba 2016
UEFA EUROPA LIGI - Kundi A
Alhamisi Novemba 3

2100 Fenerbahçe v Man United