Monday, October 24, 2016

RAIS JACOB ZUMA AWAPONGEZA MABINGWA WAPYA WA SOKA AFRIKA MAMELODI SUNDOWNS

Rais Jacob Zuma amewapongeza mabingwa wapya wa Soka Afrika timu ya Mamelodi Sundowns ambao wameshinda Ligi ya Mabingwa CAF.
Rais Zuma pia amewashukuru mashabiki wa soka na waafrika kusini wote kwa kuiunga mkono timu hiyo na hatua hiyo imezaa matunda si kwa Sundowns bali kwa taifa zima.
Sundowns wameshinda ubingwa huo licha ya kufungwa goli 1-0 na Zamalek ya Misri hapo jana usiku.

Sundowns ambao hutambulika kama Brazil ya Afrika, wameibuka na ushindi huo baada ya mchezo wa awali kuifunga Zamalek magoli 3-0, na kufanya matokeo ya jumla kuwa magoli kuwa 3-1.