Monday, October 3, 2016

SWANSEA YAMTIMUA MENEJA WAKE FRANCESCO GUIDOLIN, YAMPA KAZI KOCHA WA ZAMANI USA BOB BRADLEY!

Swansea City imemfukuza Meneja Francesco Guidolin na mara moja kumteua Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya USA Bob Bradley kushika nafasi yake.
Swansea, Klabu ya huko Wales, hivi sasa ipo juu tu ni ya Timu 3 za mkiani za EPL, Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi 1 tu kati ya 7 iliyocheza.
Mechi hiyo waliyoshinda ni Siku ya kwanza tu ya Msimu Mpya wa EPL walipoifunga Burnley 1-0.
Hivi karibuni, baada ya kutoka Sare 2-2 na Chelsea wakaja kufungwa na Manchester City na Liverpool.
Swansea hivi sasa inamilikiwa na Kampuni ya Kimarekani inayoongozwa na Stephen Kaplan na Jason Levien iliyochukua madaraka Mwezi Julai na kumrithi Meneja Francesco Guidolin ambae alishika wadhifa Mwezi Januari na awali aliwahi kuwa Kocha wa Udinese ya Italy.
Guidolin, ambae Leo anashejerekea Miaka 61, aliokoa Swansea kushuka Daraja na Mwezi Mei kupewa Mkataba wa Miaka Miwili.

Wiki yote hii kulikuwa na tetesi kuwa Guidolin atatimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Ryan Giggs au Gianfranco Zola.

Bradley, mwenye Miaka 58, amekuwa akifanya kazi na Klabu ya France Le Havre ambayo iko Daraja la Pili Ligi 2.