Thursday, October 6, 2016

TOTO WAFANYA MAZOEZI KAITABA LEO, TAYARI KUCHEZA NA WENYEJI KAGERA SUGAR JUMAMOSI.


Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Oktoba 7, 2016 kwa michezo miwili ambako Kagera Sugar itaikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja Kaitaba mkoani Kagera wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mbali ya mechi hizo za kesho, Jumamosi Oktoba 8, 2016 pia kutakuwa na michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC jijini Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikiialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza, kundi A Jumamosi Oktoba 8, kutakuwa na mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam es Salaam wakati African Sports itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.