Monday, October 17, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE - JUMANNE: RONALDO, NAPOLI WAWANIA REKODI, JUMATANO GUARDIOLA HUYOO KWA BARCELONA v MANCHESTER CITY, PSG v BASEL

BAADA ya kupotea kwa Wiki 3, Mechi za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, zinarejea tena kilingeni hapo Jumanne na Jumatano Usiku na mvuto ni kuona Cristiano Ronaldo akiwania kuweka Rekodi mpya ya Magoli wakati Napoli ikitarajia kuweka Historian a pia Pep Guardiola akitua Klabu yake ya zamani FC Barcelona.
Kwenye mojawapo ya Mechi za Jumanne, Cristiano Ronaldo anawania kuwa Mchezaji wa Kwanza kufunga Bao 100 katika Mashindano ya Klabu Ulaya.
Jumanne, Real Madrid itaongozwa na Ronaldo kucheza Mechi ya Kundi F dhidi ya Legia Warsaw Uwanjani Santiago Bernabeu na Staa, mwenye Bao 98 Ulaya, anahitaji Bao 2 tu kuweka Rekodi mpya.
Nayo Klabu ya Italy Napoli ipo kizingitini katika kuweka Rekodi mpya ya UCL ikiwa wataifunga Besiktas kwenye Mechi yao ya Kundi B ambayo itachezwa Jumatano huko Italy.
Ikiwa Napoli watashinda Mechi hiyo na Dynamo Kyiv kutoka Sare na Benfica katika Mechi nyingine ya Kundi B, basi Napoli watafuzu kutinga Raundi inayofuata ya Mtoano huku wakiwa na Mechi 3 mkononi na hiyo itakuwa Rekodi Mpya kwa kuwa Klabu ya Kwanza kufuzu hivyo.
Nae Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, ataiongoza Timu yake hapo Jumatano kutua Nou Camp kucheza na FC Barcelona ambako ndiko alijijengea Jina.
Akiwa na Barca kama Mchezaji, Guardiola alitwaa Ubingwa wa La Liga mara 6 na wa Ulaya mara 1 na alipokuwa Kocha Mkuu alizoa Makombe 14 yakiwemo Mawili ya UCL.
Mara ya mwisho kwa Guardiola kuiongoza Timu nyingine kucheza na Barca huko nou Camp ilikuwa Msimu wa 2014/15 alipokuwa na Bayern Munich na kuchapwa 3-0 kwenye Nusu Fainali ya UCL.

UEFA CHAMPIONS LIGI
Ratiba:
Jumanne Oktoba 18 

Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

KUNDI E
Bayer Leverkusen v Tottenham
CSKA v Monaco

KUNDI F
Real Madrid v Legia Warsaw
Sporting Lisbon v Borussia Dortmund

KUNDI G
Club Brugge v FC Porto
Leicester v FC Copenhagen

KUNDI H
Dinamo Zagreb v Sevilla
Lyon v Juventus

Jumatano Oktoba 19
Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

KUNDI A
Arsenal v Ludo Razgrad
Paris St Germain v Basel

KUNDI B

Dynamo Kiev v Benfica
Napoli v Besiktas

KUNDI C

Barcelona v Man City
Celtic v Borussia Monchengladbach

KUNDI D
Bayern Munich v PSV Eindhoven
FC Rostov v Atletico Madrid 


TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)