Wednesday, October 19, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO ARSENAL NA LUDOGORETS KWA MARA YA KWANZA, BARCELONA v MANCHESTER CITY

UEFA CHAMPIONS RATIBA HII LEO USIKU
Ratiba:
Jumatano Oktoba 19
Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI A

Arsenal v Ludogorets Razgrad
Paris St Germain v Basel

KUNDI B
Dynamo Kiev v Benfica
Napoli v Besiktas


KUNDI C
Barcelona v Man City
Celtic v Borussia Monchengladbach

KUNDI D
Bayern Munich v PSV Eindven
FC Rostov v Atletico Madrid

__________________________________
USIKU huu Arsenal wanacheza Mechi yao ya 3 ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMPIONS wakiwania ushindi dhidi ya Mabingwa wa Bulgaria Ludogorets Razgrad ambayo watacheza nao tena huko Sofia Mechi ifuatayo.

Baada ya kutoka Sare na Paris St-Germain katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A, Arsenal waliichapa FC Basel 2-0 na ushindi dhidi ya Ludogorets kwenye Mechi hii na ijayo utakikisha wao kufuzu hatua ya Mtoano kwenye Kundi hili ambalo wao na PSG ndio wanapewa nafasi kubwa kufuzu.

Hivi sasa Arsenal wapo kwenye wimbi zuri la ushindi kwani tangu wafungwe 4-3 na Liverpool kwenye Mechi yao ya kwanza ya EPL, Ligi Kuu England, wameshinda Mechi zao 6 zilizopita katika Mashindano yote.  


Ingawa si jina kubwa huko Ulaya, Ludogorets ni Timu ngumu kufungika na Arsenal inabidi wakaze buti kuifunga na pia kumtupia jicho Straika wao hatari kutoka Brazil Jonathan Cafu.

Hilo limemfanya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, awahimize Wachezaji wake kujituma na si kubweteka kwa kupambana na Timu isiyo na jina.

Mechi nyingine ya Kundi A hii Leo ni huko Paris, France kati ya PSG na FC Basel.


JE WAJUA?
-Arsenal na Ludogorets Razgrad hazijawahi kukutana hata mara moja!
Pep Guardiola has a laugh on the training ground as Manchester City prepare to face BarcaPEP GUARDIOLASergio Busquets in action for Barcelona against Deportivo La Coruna on SaturdayNeymar (left) and Luis Suarez arrive for a Barcelona training session on Tuesday