Thursday, October 20, 2016

UEFA EUROPA LEAGUE TATHMINI: LEO MANCHESTER UNITED vs FENERBAHCE

HII LEO Manchester United wataingia Uwanjani kwao Old Trafford Jijini Manchester kucheza Mechi yao ya 3 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI dhidi ya Klabu ya Uturuki Fenerbahce.
Ikiwa hii Leo, kwenye Mechi nyingine ya Kundi A, Feyenoord itashindwa kuifunga Zorya Luhansk huko Rotterdam, Netherlands, basi Man United wakiifunga Fenerbahce watatwaa uongozi wa Kundi A.

Timu zote, Man United na Fenerbahce, zinaingia kwenye Mechi hii zikitoka kwenye Sare za 1-1 katika Ligi za Nchini kwao wakati Fenerbahce, chini ya Kocha Mholanzi Dick Advocaat, wakitoka 1-1 na Osmanlispor Jumapili iliyopita matokeo ambao yamezidi kuwadidimizi kwenye ligi na kuleta wasiwasi kwa hatima ya Kocha wao.
Man United wao walitoka 1-1 na Liverpool huko Anfield hapo Jumatatu Usiku.
Kwenye Kundi A, Fenerbahce, ambao ndio Vinara, kwenye Mechi 2 za kwanza, walitoka Sare na Zorya Luhansk Ugenini na kushinda Nyumbani 1-0 dhidi ya Feyenoord wakati Man United walifungwa 1-0 na Feyenoord huko Rotterdam na kuichapa Zorya Luhansk 1-0 Uwanjani Old Trafford.

Akiongea hapo Jana, Meneja wa Man United Jose Mourinho alikuwa mgumu kudokeza Kikosi chake kitakachoanza hii Leo mbali ya kusema Luke Shaw atakuwemo na kudokeza Henrikh Mkhitaryan yuko fiti na yumo katika kundi la Wachezaji wanaoweza kucheza.

Pia, Majeruhi Anthony Martial na Morgan Schneiderlin, wamerejea Mazoezini na huenda wakashiriki.
Kwa upande wa Fenerbahce, inaweza ikamtumia Mchezaji wa zamani wa Man United Robi van Persie ambae hii itakuwa ni mara ya kwanza kurejea Old Trafford tangu auzwe huko Mwaka Jana.

Van Persie amerejea Uwanjani hivi karibuni baada ya kuwa majeruhi kwa muda.
Pia Fenerbahce inae Sentahafu Martin Skrtel, Mchezaji wa zamani wa Liverpoo, Mahasimu wa Man United, ambae nae alihamia huko mwanzoni mwa Msimu huu na huyu ni hakika kuanza Mechi hii akishirikiana na beki Simon Kjaer.
Katika safu yao ya mashambulizi yupo Mchezaji wa Mkopo kutoka Sunderland, Jeremain Lens, ambae ndie huwapa kasi mbele.

JE WAJUA?

-Mechi ya kwanza kabisa kwa Wayne Rooney kuichezea Man United ni Septemba 2004 dhidi ya Fenerbahce kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ambayo Rooney alipiga Hetitriki wakati Man United ikishinda 6-2.
Man United na Fenerbahce zimeshakutana mara 4 huko nyuma na Man United kushinda mara 3 na Fenerbahce mara 1 huko Instanbul wakati Man United wakichezesha Kikosi dhaifu kwenye Mechi ya Ulaya wakati wakiwa tayari wameshafuzu Kundi lao.


MAN UNITED – Mechi zao za Kundi A:
Saa za Bongo

MD 1 – Alhamisi Sep 15 – Feyenoord 0 Man United 1
MD 2 – Alhamisi Sep 29 22:05 – Man United 1 Zorya Luhansk 0
MD 3 – Alhamisi Okt 20 22:05 – Man United v Fenerbahce SK
MD 4 – Alhamisi Okt 27 2000 – Fenerbahce SK v Man United
MD 5 – Alhamisi Nov 24 2305 – Man United v Feyenoord
MD 6 – Alhamisi Des 8 2100 – Zorya Luhansk v Man United


REFA: Benoît Bastien (France)
UEFA EUROPA LIGI
Ratiba:
Alhamisi Oktoba 20
KUNDI A

Feyenoord v Zorya Luhansk 2205
Man United v Fenerbahçe 2205

KUNDI B
BSC Young Boys v Apoel Nicosia 2205
Olympiakos v FC Astana 2205

KUNDI C
FSV Mainz 05 v Anderlecht 2205
Saint-Étienne v FK Qabala 2205

KUNDI D
AZ Alkmaar v Maccabi Tel-Aviv 2205
Dundalk v Zenit St Petersburg 2205

KUNDI E
AS Roma v Austria Vienna 2205
Viktoria Plzen v Astra Giurgiu 2205

KUNDI F
KRC Genk v Athletic Bilbao 2205
Rapid Vienna v Sassuolo 2205

KUNDI G
Celta Vigo v Ajax 2000
Standard Liege v Panathinaikos 2000

KUNDI H
Konyaspor v Sporting Braga 2000
Shakt Donsk v KAA Gent 2000

KUNDI I
FC RB Salzb v Nice 2000
FK Krasnodar v Schalke 2000

KUNDI J
FK Qarabag v PAOK Salonika 1800
Slovan Liberec v Fiorentina 2000

KUNDI K
Hapoel Be'er Sheva v Sparta Prague 2000
Inter Milan v Southampton 2000

KUNDI L
Osmanlispor v Villarreal 2000
Steaua Buc v FC Zürich 2000

TAREHE MUHIMU
Droo

26/08/16: Makundi
12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32
24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16
17/03/17: Robo Fainali
Makundi
15/09/16: Mechidei 1
29/09/16: Mechidei 2
20/10/16: Mechidei 3
03/11/16: Mechidei 4
24/11/16: Mechidei 5
08/12/16: Mechidei 6
16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza
23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Marudiano
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi za Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Marudiano
24/05/17: Fainali (Friends Arena, Solna, Stockholm, Sweden)