Monday, October 24, 2016

ULIMWENGU ASEPA TP MAZEMBE, ATAKA KUTAFUTA TIMU ULAYA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, ameripotiwa kuachana na klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Habari za uhakika kutoka DRC zimeeleza kuwa, mkataba wa Ulimwengu kuichezea TP Mazembe umeshamalizika na amekataa kuongeza mwingine.
Ulimwengu, ambaye ameitumikia TP Mazembe kwa miaka mitano, ameamua kufatilia ofa mbalimbali alizopata kutoka klabu za Ulaya.
Ulimwengu amekaririwa akiwaeleza viongozi wa TP Mazembe kuwa, kwa sasa anaelekeza akili yake katika kucheza soka ya kulipwa barani

Ulaya.