Saturday, October 29, 2016

FULL TIME: MWADUI FC 0-3 SIMBA SC

Simba leo tena wameendelea kupaa kileleni baada ya kuibonda Mwadui FC 3-0 huko Shinyanga.
Bao za Simba zilifungwa na Mo Ibrahim, Bao 2, Dakika 32 na 50, na moja la Dakika ya 44 la Shiza Kichuya.
Simba sasa wamecheza Mechi 12 na wana Pointi 32 na Yanga ni wa Pili wakiwa na Pointi 24 kwa Mechi 11.
Katika Mechi nyingine za hii Leo, Mbeya City, wakiwa kwao Sokoine, waliifunga Maji Maji FC 3-2 wakati huko Mwanza Toto Africans iliichapa Mtibwa Sugar 3-2 na huko Mlandizi JKT Ruvu iliitungua Ndanda FC 1-0,
Huko Uhuru Jijini Dar es Salaam, African Lyon ilitoka Sare 1-1 na Tanzania Prisons.
VPL itaendelea tena Jumapili kwa Mechi 2 ambapo Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru, Mabingwa Watetezi Yanga wataivaa Mbao FC ya Mwanza na nyingine ni huko Mlandizi kati ya Ruvu Shooting na Stand United.