Wednesday, October 26, 2016

VPL: YANGA CHINI YA KOCHA MWAMBUSI WAIBAMIZA JKT RUVU BAO 4-0.

MABINGWA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Leo kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wameibamiza JKT Ruvu 4-0 na kuzidi kujichimbia kwenye Nafasi ya Pili sasa wakiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara Simba.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo wa kishindo kwa Yanga baada ya Mechi iliyokwisha kuitandika Kagera Sugar 6-2 huko Kaitaba Mjini Bukoba.
Yanga, wakisimamiwa na Kocha Msaidi Juma Mwambusi baada ya kujiuzulu Kocha wao Hans van de Pluijm, walipata Bao lao la Kwanza Dakika ya 6 Mfungaji akiwa Mzambia Obrey Chirwa na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili Dakika ya 58 Yanga walimtoa Straika kutoka Zimbabwe Donald Dombo Ngoma nafasi yake inachukuliwa na AmisI Tambwe ambae Dakika ya 63 aliipa Yanga Bao la Pili.

Bao la Tatu la Yanga lilifungwa na Simon Msuva katika Dakika ya 83 baada ya kumalizia Pasi safi ya Tambwe.

Tambwe aliifungia Yanga Bao la 3 Dakika za Majeruhi baada ya kuutokea Mpira uliomilikiwa na Beki wa JKT Ruvu aliejichanyanga na Kipa wake.

Hadi mwisho Yanga waliibuka kidedea 4-0.

Matokeo hayo yamezidi kuwachimbia Yanga Nafasi ya 3 kwenye VPL wakiwa na Pointi 24 kwa Mechi 10 huku Simba wakiwa kileleni wakiwa na Pointi 29 kwa Mechi 11.

VIKOSI:
YANGA:
Deogratius Munishi, Hassani Kessy, Mwinyi Haji, Vicent Bossou, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko, Saimoni Msuva [Juma Mahadhi, 89’], Haruna Niyonzima, Donald Ngoma [Amisi Tambwe, 58’], Obrey Chirwa, Deusi Kaseke

Akiba: Benno Kakolanya, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Andrew Vicent, Amisi Tambwe, Juma Mahadhi, Geofrey Mwashiuya [Geofrey Mwashiuya, 84’]

JKT RUVU: Kipao, Kindamba [Aidan, 60’], Gilla, Nurdin, Rahim, Amour [Thabit, 89’], Kisengo [Kamuntu, 46’], Nashon, Atupele, Dilunga, Mavuo