Monday, October 31, 2016

WACHEZAJI WA MAN UNITED SCHWEINI, MKHITARYAN, PHIL JONES WAREJEA KUNDINI LEO NA KUFANYA MAZOEZI.

WADAU wa Manchester United watafarijika mno na habari njema za kurejea kwenye Kikosi cha Kwanza Bastian Schweinsteiger, Henrik Mkhitaryan na Phil Jones baada ya kutoonekana kitambo.Wachezaji hao Leo walinaswa kwenye Picha wakiwa Mazoezini na Kikosi cha Kwanza huko Aon Training Complex wakijitayarisha kwa Mechi yao ijayo ya Alhamisi huko Uturuki dhidi ya Fenerbahce ikiwa ni Mechi ya Kundi lao la UEFA EUROPA LIGI.
Wakati Mkhitaryan na Phil Jones walikuwa Majeruhi, Schweinsteiger alikuwa ameondolewa toka Kikosi cha Kwanza cha Man United na Meneja Mpya Jose Mourinho tangu ashike wadhifa wake mwanzoni mwa Msimu.

The 32-year-old played 13 league games last season after being signed by Louis van GaalMara ya mwisho kwa Schweinsteiger kuichezea Man United ilikuwa ni Mwezi Machi chini ya Meneja aliepita Louis van Gaal.
Hata hivyo, Schweinsteiger hawezi kucheza Mechi za EUROPA LIGI kwa vile hakusajiliwa lakini yumo kwenye Kikosi cha kucheza EPL, Ligi Kuu England na hivyo anaweza kucheza Jumapili ijayo Ugenini na Swansea City hasa kwa vile Ander Herrera ataikosa Mechi hiyo akitumikia Kifungo chake baada ya kupokea Kadi Nyekundu Jumamosi walipotoka 0-0 na Burnley.
Tangu ajiunge na Man United Julai 2015 akitokea Bayern Munich kwa Dau la Pauni Milioni 14.4, Schweinsteiger ameichezea Man United Mechi 31.