Wednesday, October 19, 2016

WAYNE ROONEY AJITETEA NA KUSEMA BADO UWEZO WA SOKA ANAO KWA SANA!

KEPTENI wa Manchester United na England, Wayne Rooney, amekiri kuwa sasa anakabiliwa na changamoto mpya katika Maisha yake ya Soka lakini amesisitiza bado hajaisha na Soka lipo sana kwake.
Rooney, ambae Jumatatu atatimiza Miaka 31, alitoa kauli hiyo alipoongea na Wanahabari mara baada ya Man United kutoka 0-0 na Liverpool Jumatatu iliyopita huko Anfield Gemu ambayo yeye alianzia Benchi. Rooney aliieleza Gemu na Liverpool kuwa ilikuwa muhimu wasifungwe hasa kwa vile wanakabiliwa na Mechi ngumu zijazo dhidi ya Fenerbahce, Chelsea na Manchester City.
Rooney, ambae kwa sasa akiwa na Man United amechezea Gemu 4 akitokea Benchi, amesisitiza kuwa yeye yupo tayari wakati wowote akiitwa kucheza.
Ameeleza: “Napenda kufikiri naweza kucheza kila Gemu lakini ni wazi ni uamuzi wa Meneja na naheshimu hilo. Nitakuwa tayari nikihitajika. Natimiza Miaka 31 Wiki ijayo lakini bado nina Soka jingi lililobaki kwangu!”

JE WAJUA?
-Rooney ameichezea Man United Mechi 529 na Kufunga Magoli 246 [Amebakisha Bao 3 tu kuikamata Rekodi ya Mfungaji Bora katika Historia ya Man United ya Bao 249 zilizofungwa na Sir Bobby Charlton aliecheza Mechi 758 kati ya Miaka ya 1956 na 1973]

Kuhusu matarajio ya Man United Msimu huu, Rooney amedai kuwa chini ya Jose Mourinho watatoa upinzani mkali kwenye mbio za Ubingwa.