Friday, October 28, 2016

WAZIRI NCHEMBA AFANIKISHA KOCHA PLUIJM KURUDI YANGA!

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, amefanya jitihada kubwa zilizofanikiwa kumrudisha Kocha Hans van de Pluijm Klabuni Yanga baada ya kujiuzulu Majuzi.
Kocha Pluijm alijiuzulu mapema Wiki hii baada kuibuka habari kuwa Yanga inataka kumuajiri Kocha Mzambia Lwandamina aliekuwa akiifundisha ZESCO ya huko kwao.
Jumanne, ikiwa ni Siku moja kabla Yanga kucheza na JKT Ruvu waliyoifunga 4-0 kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakiwa chini ya usimamizi wa Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Pluijm alienda Mazoezini mwa Yanga na kuwaaga Wachezaji.
img-20161028-wa0005
Lakini Leo, baada ya jitihada kubwa za Waziri Nchemba, Yanga imemwandikia Pluijm Barua ya kukataa kujiuzulu kwake na sasa inaaminika Kocha huyo tayari amerejea kwenye Timu.
Kesho Jumamosi, Kocha Pluijm anatarajiwa kuiongoza Yanga Uwanjani Uhuru kuikabili Mbao FC katika Mechi ya VPL.

VPL
Ratiba/Matokeo:
Ijumaa Oktoba 28

Kagera Sugar 2 Azam FC 3
 

Jumamosi Oktoba 29
Yanga v Mbao FC
Mwadui FC v Simba
Mbeya City v Maji Maji FC
Toto Africans v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v Ndanda FC

Jumapili Oktoba 30
Ruvu Shooting v Stand United
African Lyon v Tanzania Prisons