Wednesday, November 30, 2016

ATHIBITISHWA, SOUTHGATE NI MENEJA MPYA ENGLAND!

FA, The Football Association, Chama cha Soka England, kimetangaza Gareth Southgate ndie Meneja Mpya wa Timu ya Taifa ya England.
Southgate, mwenye Miaka 46, amesaini Mkataba wa Miaka Minne.
Southgate aliteuliwa kuwa Meneja wa Muda wa England Mwezi Septemba baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce na kusimamia Mechi 4 ambazo walishinda 2 na Sare 2.

Akiongea baada ya kuthibitishwa hii Leo, Southgate alisema: “Nasikia fahari kubwa kuwa Meneja wa England. Najua kupata kazi ni jambo moja na kuwa na mafanikio ni kitu kingine kabisa!”

Mkataba wa Southgate na FA haukuwekwa wazi lakini inaaminika atavuna Pauni Milioni 2 kwa Mwaka ikiwa ni mara 4 ya Mshahara aliokuwa akilipwa wakati akiwa Bosi wa Timu ya Taifa ya England ya Vijana chini ya Miaka 21, U-21.

Southgate hana uzoefu mkubwa kama Meneja baada ya kuiongoza Middlesbroughna hiyo U-21 tu na anakuwa Meneja wa kwanza Mwingereza wa Timu ya Taifa ya England tangu Kevin Keegan ajiuzulu Mwaka 2000.

Mechi zinazofuata kwa England ni Mwezi Machi Ugenini na Mabingwa wa Dunia Germany ikiwa ni Mechi ya Kirafiki na kufuatia na ile ya Uwanjani Wembley na Lithuania ikiwa ni ya Kundi lao kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2018n huko Russia.