Tuesday, November 15, 2016

BASTIAN SCHWEINSTEIGER AZUNGUMZA NA KLABU YA USA CHICAGO FIRE UHAMISHO WAKE

Image result for Bastian Schweinsteiger  MLSKIUNGO wa Manchester United Bastian Schweinsteiger amekutana na Klabu inayocheza MLS huko Marekani Chicago Fire na zipo kila dalili atahamia huko Mwezi Januari.
Bastian Schweinsteiger hajaichezea Mechi yeyote Man United chini ya Meneja Jose Mourinho Msimu huu.
Habari toka ndani ya Man United zimetoboa kuwa Nahodha huyo wa Germany mwenye Miaka 32 alishapewa ruhusa ya kuongea na Klabu yeyote inayomtaka.
Inaaminika Schweinsteiger anapendelea kucheza huko USA na hivi Juzi alikutana na Kocha wa Chicago Fire Veljko Paunovic.
Hivi karibuni, Schweinsteiger alirejeshwa kufanya Mazoezi na Kikosi cha Kwanza cha Man United baada ya awali kuzuiwa na Mourinho.
Hata hivyo haitarajiwi kama Mourinho atampa Namba kwenye Mechi Mjerumani huyo alieibebesha Kombe la Dunia Nchi yake huko Brazil Mwaka 2014.
Schweinsteiger, aliejiunga na Man United kutoka Bayern Munich kwa Dili ya £14.4m Julai 2015, hajaichezea Timu hiyo tangu Mwezi Machi walipoifunga Man City 1-0 wakiwa chini ya Meneja aliemtangulia Mourinho, Louis van Gaal.
Schweinsteiger ameichezea Man United Mechi 31