Sunday, November 6, 2016

BORUSSIA DORTMUND 5-2 HAMBURG: PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG NI HATARI SANA...ATUPIA NNE WAVUNI !!


Pierre-Emerick Aubameyang amerejea katika kikosi cha Borussia Dortmund kwa kishindo kwa kupachika magoli manne, na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Hamburg.
Aubameyang, 27, raia wa Gabon aliwekwa nje ya kikosi siku ya jumatano katika mchezo walioshinda wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sporting Lisbon kutokana na kuwepo kwa tofauti za ndani ya klabu hiyo.

Aubameyang alirejeshwa kikosini na kocha Thomas Tuchel jumamosi na kufunga hat-trick ndani ya dakika 23 za kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza goli la nne dakika chache tu baada ya kuanza kipindi cha pili.

Katika mchezo huo pia Ousmane Dembele aliifungia Borussia Dortmund goli, huku magoli ya Hamburg yote yakifungwa na Nicolai Muller.