Sunday, November 20, 2016

CRISTIANO RONALDO AITEKETEZA ATLETICO MADRID

DABI ya Jiji la Madrid huko Spain, ambayo Jina la ubatizo ni ‘El Derbi MadrileƱo’, kati ya Atletico Madrid na Real Madrid ilichezwa Jana kwenye Uwanja wa Vicente Calderon na Vinara wa La Liga Real kuibuka kidedea kwa Bao 3-0 ambazo zote zilifungwa na Cristiano Ronaldo.
Hiyo ikiwa ni Dabi ya mwisho kuchezewa Uwanjani Vicente Calderon kwani Msimu ujao Atletico wanahamia Uwanja mpya na Ronaldo ndie alikuwa mwiba akipiga Hetitriki yake ya 39 katika Maisha yake ya Soka.

Ronaldo alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 23 kwa Frikiki na Bao la Pili Dakika ya 71 kwa Penati na kumaliza la mwisho Dakika ya 77.Ushindi huo umewaweka Real Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili FC Barcelona ambao mapema Jana walitoka 0-0 na Malaga na pia kuwabwaga Atletico kuwa Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Real.
Cristiano Ronaldo celebrates scoring their first goal with team