Tuesday, November 15, 2016

CRISTIANO RONALDO APANDA CHATI UFUNGAJI BORA ULAYA KATIKA HISTORIA!

Cristiano Ronaldo started his career with Sporting Lisbon, where he played with Phil BabbJumapili Usiku Cristiano Ronaldo alifunga Bao 2 wakati Nchi yake Portugal ikiifunga Latvia katika Mechi ya Kundi B la Nchi za Ulaya za kusaka nafasi za kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 na kufikisha Bao 68 za Mechi za Kimataifa za Nchi.
Idadi hiyo imemfanya akae Nafasi ya 4 katika Ufungaji Bora katika Historia kwa Nchi za Ulaya akifungana na Robbie Keane na Gerd Müller.

Bao hizo 68 za Ronaldo zimetokana na Mechi 136 alizoichezea Portugal na sasa anawinda kumkamata Miroslav Klose mwenye 61 alie Nafasi ya 3 na kisha Sándor Kocsis mwenye 75 na ni wa Pili.
Anaeshikilia Rekodi ni Ferenc Puskas mwenye Bao 84.


ULAYA - WAFUNGAJI BORA KATIKA HISTORIA:
Ferenc Puskás (Hungary & Spain) – Goli 84 Mechi 89
Sándor Kocsis (Hungary) – Goli 75 Mechi 68
Miroslav Klose (Germany) – 71 Mechi 137
Cristiano Ronaldo (Portugal) – 68 Mechi 136
Gerd Müller (West Germany) – 68 Mechi 62
Robbie Keane (Republic of Ireland) – 68 Mechi 146
Zlatan Ibrahimović (Sweden) – 62 Mechi 116
Imre Schlosser (Hungary) – 59 Mechi 68
David Villa (Spain) – 59 Mechi 97
Jan Koller (Czech Republic) – 55 Mechi 91
Joachim Streich (East Germany) – 55 Mechi 102
Wayne Rooney (England) – 53 Mechi 117
Poul Nielsen (Denmark) – 52 Mechi 38
Jon Dahl Tomasson (Denmark) – 52 Mechi 112
Lajos Tichy (Hungary) – 51 Mechi 72
Hakan Sükür (Turkey) – 51 Mechi 112
Thierry Henry (France) – 51 Mechi 123
Robin van Persie (Netherlands) – 50 Mechi 101