Sunday, November 6, 2016

DONALD TRUMP AONDOLEWA JUKWAANI BAADA YA KUTOKEA TISHIO LA USALAMA WAKE, NJEMA MOJA CHINI YA ULINZI!


Mgombea wa Republican Donald Trump amelazimika kuondolewa haraka jukwaani na maafisa usalama katika mkutano wake wa hadhara huko Reno, Nevada baada ya kutishiwa usalama wake.
Katika tukio hilo mwanaume mmoja aliyekuwa amebeba bango linalosema Republican wanampinga Trump, alikamatwa na maafisa usalama baada ya kusema kuwa ana silaha, jambo ambalo baadaye ilibainika kuwa si kweli.

Mgombea huyo wa Republican baadaye alirejea jukwaani baada ya kuhakikishiwa usalama wake, na kusema kuwa amejipanga kwenda kwenye majimbo ambayo ni ngome ya chama cha Democratic.

Donald Trump akishikwa na afisa usalama na kuondolewa jukwani

Maafisa usalama wakimuondoa Trump jukwaani huku wakimkinga asiweze kudhuriwa

Mwanaume aliyedai kuwa na silaha akiwa chini ya ulinzi akisindikizwa na maafisa usalamaChini ya Ulinzi mkali wa polisi