Sunday, November 6, 2016

EPL LEO HAPATOSHI...DABI YA LONDON YA KASKAZINI...ARSENAL v TOTTENHAM HOTSPUR..KANE, MOUSA DEMBELE WAKO FITI!

LEO ni hekaheka huko Emirates Jijini London wakati wa Dabi ya London ya Kaskazini kati ya Arsenal na Tottenham Hotspur ikiwa ni Mechi muhimu ya EPL, Ligi Kuu England.
Timu zote hizi zimetoka kwenye Mechi za Kati-Wiki za UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, ambazo Arsenal wakicheza Ugenini na Ludogorets Razgrad walitoka nyuma 2-0 na kushinda 3-2 wakati Spurswakitunguliwa 1-0 na Bayer Leverkusen huko Wembley.
Arsenal wapo Nafasi ya 3 kwenye EPL wakiwa na Pointi 23 wakiwa nyuma ya Vinara City wenye Pointi 24 na Chelsea wenye 25.
Ushindi kwa Arsenal utawaweka kileleni hasa ikiwa hii Leo Liverpool watashindwa kuyapiku Mabao ya Arsenal wakiifunga Watford huko Anfield.
Spurs wao wako Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 20.
Arsenal watatinga kwenye Mechi hii wakiwa na hatihati kuhusu Wachezaji wao Watano ambao wana maumivu.
Watano hao ni Theo Walcott, Santi Cazorla, Nacho Monreal, Hector Bellerin na Kieran Gibbs.

Lakini Arsenal itakuwa nae tena Kiungo Granit Xhaka ambae amemaliza Kifungo chake cha Mechi 3 baada ya kula Kadi Nyekundu kwenye Mechi na Swansea.
Hata hivyo Arsenal haitakuwa nao Majeruhi Lucas Perez (Enka), Per Mertesacker na Danny Welbeck wote wakiwa na matatizo ya Goti.
Kwa Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino mtihani mkubwa kwake ni kuamua kama Straika Harry Kane aanze Dabi hii baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 7 akiuguza Enka yake.
Pia Spurs watamtathmini Mousa Dembele Dakika za mwisho ili kujua kama yuko fiti au la kutokana na tatizo.la Mguu.
Wachezaji wa Spurs ambao ni Majeruhi na watakosekana kabisa ni Erik Lamela na Toby Alderweireld na pia Moussa Sissoko ambae yupo Kifungoni.

JE WAJUA?
*Spurs wameshinda mara moja tu katika Mechi 26 zilizopita walizocheza Nyumbani kwa Arsenal.Spurs wanapanga kuhamia kwenye Uwanja wao mpya mwaka 2018.