Sunday, November 27, 2016

FULL TIME: MANCHESTER UNITED 1 v 1 WEST HAM UNITED, HAKUNA MBABE OLD TRAFFORD ..SARE!MANCHESTER UNITED wametoka Sare yao ya 4 mfululizo ya EPL, Ligi Kuu England, Uwanjani kwao Old Trafford walipotoka 1-1 na West Ham.
Sekunde 90 tu tangu Mechi ianze, West Ham walifunga Bao kwa Frikiki ya Dimitri Payet kuunganishwa na Diafra Sakho na kuwapa Bao.
Man United walitulia na kukontroli Gemu na kusawazisha Bao Dakika ya 21 kufuatia muvu ya Pasi 22 ikiguswa na kila Mchezaji wa Man United na kisha kumfikia Paul Pogba na kummiminia Zlatan Ibrahimovic aliefunga kwa Kichwa.

Mabao hayo yalidumu hadi Haftaimu lakini matukio makubwa katika Kipindi cha Kwanza hicho ni Paul Pogba kupewa Kadi ya Njano na Refa Jon Moss kwa madai ya kujiangusha na Kadi hiyo kumfanya Pogba sasa apate Kifungo cha Mechi 1 kwa kuwa amezoa Kadi za Njano 5 na ataikosa Mechi ifuatayo Jumatano ya EFL CUP dhidi ya hao hao West Ham Uwanjani Old Trafford.

Tukio hilo lilimkasirisha sana Jose Mourinho na kuibutua Chupa ya Maji kwenye Eneo lake la Ufundi na Refa Moss kumtoa Uwanjani aende Jukwaani kwa Watazamaji akimwacha Msaidizi wake Lui Faria kukaimu.
Mechi inayofuata ya EPL kwa Man United ni Ugeni huko Goodison Park dhidi ya Everton ambao Leo walichapwa 1-0 huko Saint Mary
kwa Bao la Sekunde ya 43 tu la Charlie Austin walipocheza na Southampton.

Jose Mourinho nae amembiwa akauangalizie kwa mashabiki na Refa

JE WAJUA?
-Refa Jon Moss ashawahi kumtoa nje Jose Mourinho akae Jukwaani wakati ni Meneja wa Chelsea.
-Mourinho alimkabili tena Refa huyo Siku hiyo hiyo na FA kumfungia kukanyaga Uwanjani.
-Refa Jon Moss ameichezesha Man United Mechi 13 na kushinda 11 na Sare 2

1-11-0